Uganda yatafuta ufadhili wa China kwenye ujenzi wa bomba.

Serikali ya Uganda ipo katika hatua za mwisho za majadiliano na wafadhili kutoka China kuisaidia kufadhili mradi wenye utata wa bomba la mafuta ghafi.

Hayo yamesemwa jana na Irene Bateebe katibu katika wizara ya Nishati nchini Uganda.

Akizungumza na shirika la habari la AFP, Bateebe ameeleza kuwa wanafanya majadiliano ya mwisho na washirika wao wa China kuwapa nusu ya fedha za ufadhili wa mradi huo, na kwamba mazungumzo hayo yatakamilika mwezi Oktoba.

Kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies inaongoza ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kugharimu mabilioni yad ola kuwezesha Uganda kusafirisha mafuta yake ghafi hadi bandari ya Tanzania, umbali wa kilomita 1, 445.

Mradi huo umekosolewa pakubwa na watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati wa mazingira wanaosema utadhuru mifumo ya ikolojia na pia maisha ya maelfu ya watu.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii