Afrika Mashariki wenyeji AFCON 2027

Hatimaye Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limeipa nafasi Afrika Mashariki kupitia nchi za Tanzania, Uganda na Kenya kuwa mwenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ kupitia vyanzo vyake vya habari, Tanzania, Uganda na Kenya zimekubaliwa kuwa mwenyeji wa AFCON 2027, baada ya kupigiwa kura na wajumbe wa CAF.

Taarifa ya TFF iliyochapishwa katika Kurasa zake za Mitandao kuhusu kukubaliwa kwa nchi hizo kuwa mwenyeji wa AFCON 2027, imeandikwa ‘ACCEPTED!!!’. Katika hatua nyingine Morocco imetajwa kuwa mwenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2025’ ikipokea kijito kutoka kwa Ivory Coast itakayokuwa mwenyeji wa Fainali za 2023 zitakzofanyika mapema mwaka 2024.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii