Estonia yahimiza wanachama wa NATO kuongeza bajeti ya Ulinzi

Waziri Mkuu wa Estonia Kaja Kallas ameyahimiza mataifa mengine wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, kuongeza bajeti za ulinzi kwa kuiga mfano wa nchi tatu za kanda ya Baltiki.

Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa kila mwaka juu ya usalama wa eneo la Baltiki ulianza jana nchini Estonia, Bibi Kallas amesema ni muhimu kwa nchi nyingine za NATO kutanua matumizi ya sekta ya ulinzi kwa sababu kitisho cha usalama kimeongezeka na vita vimerejea barani Ulaya.

Mkutano huo wa mataifa ya Baltiki yanayojumuisha Latvia, Lithuania na Estonia, unafanyika chini ya kiwingu cha wasiwasi mkubwa wa usalama kwenye eneo hilo tangu Urusi ilipoivamia kijeshi Ukraine mwaka jana.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii