Ramadhani Brothers Kutoka Tanzania Watinga Nusu Fainali American Got Talent, Kuwania Sh Bilion 2.4


Ni baada ya kuvuka Nusu Fainali katika Mashindano hayo ya Kusaka Vipaji ambapo sasa watashindana na The 82nd Airborn Division All American Chorus, Avantgardey, Chibi Unity, Anna DeGuzman, Putri Ariani, The Mzansi Youth Choir, Murmuration, Ahren Belisle, Lavender Darcangelo, na Adrian Stoica & Hurricane hapo Septemba 26, 2023

Wawili hao wanajitambulisha kwa jina Ramadhani Brothers wamesifiwa na Majaji wote wa America's Got Telent (AGT) akiwemo Jaji Mkuu Simon Cowell aliyesema "Onesho lao lilikuwa la kushangaza na la kipekee sana, lilikuwa gumu na la kutisha sana. Maoni yangu: Onesho hili linapaswa kufika Fainali, na ninaamini ni onesho la ushindi"

Mbali na AGT, Ramadhani Brothers wameshashiriki mashindano mengine kama La France a un Incroyable Talent na kufika fainali, Australia’s Got Talent walipata heshima ya "Golden Buzzer", Romanii Au Talent walifika nusu fainali na Got Talent All-Stars ambayo pia walifika fainali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii