Taarifa kutoka Yanga ni kuhusu majeruhi ya Lomalisa

Mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa Mutambala anatarajiwa kuwa nje kwa wiki moja baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex jana Jumatano, ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0


Lomalisa alishindwa kuendelea na mchezo huo kwenye kipindi cha pili baada ya kuchezewa rafu mbaya na Hashim Manyanya wa Namungo Fc

Ilikuwa rafu ambayo pengine ilistahili mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kumuonyesha Manyanya kadi nyekundu lakini hata hivyo alitoa kadi ya njano

Ni wazi Lomalisa huenda akakosa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi dhidi ya Al Merrikh ambao utapigwa Septemba 30 katika uwanja wa Azam Complex

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii