Jimbo la British Columbia lililopo karibu na bahari ya Pacific linajiandaa kwa wimbi la joto kali ambalo huenda likachochea zaidi moto unaoendelea kuwaka. Waziri wa Ulinzi wa Canada Bill Bliar kupitia ujumbe wakwa kwenye mtandao wa X, uliokuwa unajulikana kama Twitter amesema kwambawako pamoja na watu wa maeneo ya Kaksazini magharibi mwa nchi wakati wakikabiliana na moto huo.
Ameongeza kusema kwamba jeshi lililotumwa litasaidia katika kuuzima moto, kusafirisha watu, pamoja na kupanga mikakati mingine ya kudhibiti hali. Idadi kamili ya wanajeshi waliotumwa haijatolewa ingawa mamia wengine walitumwa awali kwenye majimbo mengine manne katika miezi ya karibuni, ili kukabiliana na moto, wakishirikiana na karibu zimamoto 11,000, wakiwemo 5,000 kutoka mataifa ya kigeni.