Tory Lanez Ahukumiwa Miaka 10 Jela Kwa Kumpiga Risasi The Stallion

Nyota huyo wa Hip Hop na R&B mwenye asili ya Canada amehukumiwa kifungo baada ya kupatikana na hatia ya makosa 3 ikiwemo kumpiga Risasi Rapa wa Kike #MeganTheeStallion Julai 2020, huko #HollywoodHills

Licha ya #ToryLanez kukana Mashtaka yote (Kushambulia kwa Kutumia Bunduki, Kubeba Bunduki Isiyo na Usajili na Kutumia Bunduki kwa Uzembe), Mahakama ilimtia hatiani kwa makosa yote 3

Megan Thee Stallion alimshutumu Lanez kwa kumshambulia kwa Risasi Mguuni baada ya kutoka nje ya gari walilokuwa wamepanda baada ya kutokea Mabishano kati yao

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii