Basi la Ngasere lapata ajali Mpwapwa

Abiria wa Basi la Ngasere lililokuwa likisafiria kutoka Wilayani Mpwapwa kwenda jijini Dodoma, wanadaiwa kunusurika kifo, baada ya usafiri huo kupata ajali katika eneo la Kijiji cha Chunyu, Wilayani humo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wamesema Basi hilo likiwa safarini lilianza kuyumba ghafla na kupinduka, huku wakidai kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha isipokuwa watu wachache kupata majeraha madogo.

Aidha, wameushauri uongozi wa Kampuni hiyo kubadilisha magari au kuyafanyia ukarabati kutokana na uchakavu mkubwa wa baadhi ya usafiri huo unaofanya safari zake kati ya Dodoma, Mpwapwa na baadhi ya Vijiji.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii