Mama Mzazi wa Rais wa Shirikisho la soka la Hispania Luis Rubiales amelazwa baada ya hali yake kubadilika wakati akiwa kwenye mgomo wa kula kufuatia tuhuma za “busu la Kombe la Dunia” zinalomkabili kijana wake.
Angeles Bejar alijifungia Kanisani juzi Jumatatu na kusema kuwa hatokula wala kutoka mpaka matatizo ya kijana wake yatakapopata suluhisho.
Rubiales ambaye FIFA imesimamisha kazi anakabiliwa na makosa ya kumpiga busu mdomoni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania (wanawake) Jenni Hermoso.
Mchungaji mmoja aliyejitambulisha kama Father Antonio amelieleza shirika la habari la Reuters kuwa Mama huyo alitakiwa kuzungumza na waandishi wa habari leo, hata hivyo kutokana na hali yake mkutano huo ulifutwa na amepelekwa hospitali katika mji wa Motril.
“ Amekuwa hajisikii vizuri kutokana na joto na mengineyo,”
”Miguu yake imevimba, amechoka sana, pia ni mtu mwenye woga sana” alisema Father Antonio.