Wafanyakazi 11 Wa Soka La Hispania Wajiuzulu Kufuatia Sakata La Busu

Wafanyakazi 11 katika soka la Hispania wamejiuzulu kufuatia sakata la busu lililotokea katika sherehe za Kombe la Dunia la Wanawake huko Sydney, Australia.

Kati ya waliojiuzulu wamo makocha wote wa timu ya taifa ya wanawake kasoro kocha Mkuu Jorge Vilda.

Vilda ambaye pia ana tuhuma za kuwa na tabia zisizofaa kwa wachezaji na wafanyakazi wakike bado yupo kwenye nafasi yake.

Katika tamko lao la pamoja lililotolewa muda mfupi uliopita wafanyakazi hao wamesema wanakemea vikali kitendo kilichofanywa na Rais wa shirikisho la soka la Hispania Luis Rubiales.

Vilevile wamesema wanamsapoti mchezaji Jenni Hermoso na kuzikosoa kauli zisizokubalika zilizotolewa na Rubiales.

Wafanyakazi hao wameamua kuonyesha ushirikiano na timu ya taifa ya wanawake ya Hispania ambayo imesema kuwa haitocheza tena mpaka Rubiales asiwepo kabisa kwenye kazi yake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii