Vinara wa Ligi Kuu Ya NBC Tanzania bara timu ya Yanga imeendelea na wimbi la ushindibaada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Tanzania Polisi mchezo uliopigwa katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid, jijini Arusha.
Shujaa wa Yanga ni winga mchachari aliyetokea benchi Dickson Ambundoaliwanyanyua washabiki wa Yanga dakika ya 64 akimalizia pasi ya Fiston MayeleKwa matokeo hayo Yanga wamefikisha Pointi 35 wakiwa wamecheza mechi 13 na kuwacha Simba kwa tofauti ya Pointi 10 ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na Pointi 25 kwa mechi 12 walizocheza