Timu ya Taifa ya Tanzania (TaifaStars), imepangwa Kundi E katika makundi ya kufuzu Kushiriki Michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2026
Katika droo iliyochezeshwa leo makundi 9 yenye timu 6 yamepangwa, Tanzania ipo Kundi moja na timu za Taifa za Zambia, Morocco, Congo, Niger na Eritrea
Mechi za Kufuzu zitaanza Novemba 2023, na Washindi wa kila Kundi watafuzu moja kwa moja kwenda kushiriki Kombe la Dunia katika nchi za Canada, Mexico na Marekani
Timu 4 bora zilizoshika nafasi ya pili (Kutoka Makundi) zitacheza mechi za mtoano za CAF. Washindi watacheza mechi za mtoano za FIFA na timu itakayoshinda itaenda kushiriki Kombe la Dunia kama timu ya 10 kutoka Afrika