Wilson Oruma "Robertinho hampendi Chama tangu siku ya kwanza"

Wakati vuguvugu la kiungo wa Simba Clatous Chotta Chama likizidi kuchukua nafasi katika midomo ya wapenda soka nchini.

Mchambuzi wa Michezo kutoka EFM ametoa kauli inayoonesha kuwa Chama hatakiwi na mwalimu Robertinho katika kikosi cha Simba SC.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Oruma ameandika;

"Clatous chota Chama sio Kipenzi Cha ROBERTINHO tangu siku ya Kwanza

Na kwa hiki kinachoendelea yeye anatakiwa tu Kuomba usajili wa Kina Aubin Kramo Kouame usi Click.

Unasema Mkataba wako ulikuwa ni Mwaka Mmoja? Fine tuonyeshe,sisi tunao wa Miaka 2 na ni huu hapa. Simple hivyo."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii