Wito wa Arsene Wenger kwa mabadiliko katika kanuni za kuotea unaonekana kuwa na matunda, huku shirikisho la soka la dunia, FIFA, likipanga kujaribu mapendekezo mapya.
Wenger amekuwa akisisitiza mabadiliko katika kanuni za kuotea. Meneja huyo wa zamani wa Arsenal amehudumu kama Mkuu wa Maendeleo ya Soka ya Kimataifa ya FIFA tangu aondoke Gunners mwaka 2018. Italy Offers Colosseum for Elon Musk and Mark Zuckerberg’s Fight Keep Watching Kulingana na utaratibu wa sasa, mchezaji mara nyingi huchukuliwa kuwa kaotea ikiwa sehemu yoyote ya mwili wake inayoweza kugusa mpira iko mbele ya beki wa mwisho. Hii mara nyingi imepelekea uchunguzi mrefu wa Video Assistant Referee (VAR), na magoli kutengwa kwa sababu ya tofauti ndogo kabisa.