Rais wa Barcelona Afichua Klabu Hiyo Bado Inamlipa Messi Mshahara Miaka Miwili Baada ya Kuondoka

Barcelona bado inamlipa Lionel Messi zaidi ya miaka miwili baada ya kuondoka klabuni na itaendelea kufanya hivyo hadi angalau 2025. 


Katika mahojiano na Cadena SER, Laporta aliulizwa ikiwa Barca bado inadaiwa pesa na mchezaji na alijibu kuwa "kila kitu kimekubaliwa naye". "[Je] tunadaiwa pesa yoyote na Messi? Kitu pekee tunachodai ni malipo yaliyopangwa na bodi ya awali ya klabu. Hii inaleta malipo yaliyosalia ambayo yatakamilika mwaka 2025. Tunalipa kila kitu kwa uaminifu," Laporta alisema. 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii