Klabu ya Yanga SC imemuuza Mchezaji Feisal Salum (Fei Toto) kwa Klabu ya Azam FC kwa dau ambalo imesema halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
Siku chache zilizopita, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa Viongozi wa #Yanga kulimaliza suala la #FeiToto, alipowaalika Ikulu kwenye hafla ya Chakula kuwapongeza kwa kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF)