usajili wa Harry Kane watia presha

Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amewaambia mabosi wa timu hiyo kuhakikisha wananasa saini ya Mshambuliaji kutoka England na Tottenham Hotspur Harry Kane kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Barani Ulaya.

Kane ameingia kwenye miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake huko Spurs na jambo hilo limeibua vita kali kutoka kwa klabu zinazohitaji saini yake, ikiwamo Manchester United.

Real Madrid imetangaza itaachana na Mshambuliaji wake nguli, Karim Benzema kwenye majira haya ya kiangazi, hivyo watahitaji mrithi wake kwa haraka na Meneja Ancelotti anadhani Kane ni mtu sahihi zaidi.

Meneja huyo Mtaliano juma lililopita alikutana na rais wa klabu, Florentino Perez na meneja Jose Angel Sanchez huko kwenye uwanja wa mazoezi wa Real Madrid na kujadili juu ya mambo machache ya usajili wa dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kane amekuwa na kiwango bora kwa misimu kadhaa ingawa ameshindwa kutwaa mataji makubwa na kikosi chake cha Spurs na anataka kuondoka kwenda kusaka mafanikio kwengine.

Mafanikio makubwa kwake ni kucheza fainali ya kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii