Fiston Mayele Aibuka Mfungaji Bora Kombe la Shirikisho

Mshambuliaji na mfumaniaji nyavu wa Young Africans SC Fiston Kalala Mayele amezawadiwa tuzo ya mfungaji Bora wa michuano ya Shirikisho Barani Afrika katika msimu wa 2022/23 baada ya kuibuka kinara wa upachikaji magoli katika mashindano hayo yaliyofika tamati jana Jumamosi Juni 3.


Mayele ananyakua tuzo hiyo akiwa kinara wa ufungaji akiwa na mabao Saba huku akishuhudia Ubingwa ukienda kwa USM Algiers.


Katika msimu wa 2022/23 Mayele amefunga jumla ya magoli 15 katika michuano yote ya CAF aliyoshiriki kwa maana ya Klabu Bingwa na Shirikisho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii