Manchester United wameshuhudia ofa yao ya awali ya pauni milioni 40 kwa kiungo wa kati Mason Mount kukataliwa na Chelsea.
Inaripotiwa kuwa The Blues wanashikilia dau la juu zaidi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.
Mount ambaye mkataba wake Stamford Bridge utamalizika 2014 anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto baada ya pande zote mbili kushindwa kukubaliana juu ya kuongezwa upya.
Man United wamekuwa wakimpenda Mount kwa muda mrefu huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 akipendelea kuhamia Old Trafford.
United hata hivyo watalazimika kuongeza jitihada zao ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya Chelsea kwa mchezaji huyo.