Mitandao inaripoti kwamba Cristiano Ronaldo amesaini makubaliano ya kabla ya ndoa (pre-nup agreement) ambapo imeelezwa kwamba, kama ikitokea wakaachana, nyota huyo wa Ureno atakuwa akimlipa mpenzi wake Georgina Rodriguez kiasi cha (€100,000) zaidi ya TSh. Milioni 257 kila mwezi katika kipindi chote cha maisha yake.
Ronaldo na Georgina wana watoto wawili pamoja huku wakilea familia ya watoto watano ambao Ronaldo aliwapata nje.