Mkali wa Afrobeats, David Adeleke, almaarufu Davido, amefichua kuwa mtoto wake marehemu, Ifeanyi, ana kaka mdogo anayeitwa Dawson.
Mwimbaji huyo alifichua haya katika mahojiano ambayo yalifanyika siku ya Jumanne usiku.
Pia alifichua kuwa aliwataja binti zake, Imade na Hailey baada ya marehemu mama yake na kuongeza kuwa Hailey ni mfano wa mama yake.
Alisema, “Niliwaita wote wawili [binti zangu] kwa jina la mama yangu. Hailey ndiye mfano halisi wa mama yangu; binti yangu wa pili, yeye ni kama mama yangu. Ni kichaa. Ni kama aliingia hapa kama vile alikuja naye.
“Mimi pia nina mtoto wa kiume. Kama vile Ifeanyi ana kaka mdogo. Jina lake ni Dawson. Anaishi London hivi sasa."
Kumbuka mwimbaji huyo hivi majuzi alifichua jinsi ambavyo bado hutokwa na machozi kila wazo la marehemu mwanawe linapoibuka.