DJ ZINHLE AKIRI HAYUKO TAYARI KUFIKA DURBAN BAADA YA KIFO CHA A.K.A

DJ Zinhle hayuko tayari kutembelea Durban hivi karibuni kufuatia kifo cha baba wa mtoto,wake  Kiernan Forbes maarufu A.K.A 

Ikumbukwe kwamba rapa AKA alipigwa risasi na kuuawa mjini Durban tarehe 10 Februari 2023.

DJ Zinhle na marehemu AKA walishirikiana kwa uzuri sana katika malezi yam toto wao Kairo Forbes licha ya kuwa hawakuwa Pamoja katika mahusiano.

Zinhle anatarajiwa kutumbuiza katika hafla ya Fact Durban Rocks huko Durban July mwaka huu,lakini kifo cha mpenzi wake wa zamani kitabadilisha mipango yake kwani anadai kuwa hayuko tayari kutembelea Durban.



"Siwezi kuwadanganya nyie, siko tayari kwa Durban. Kihisia, siko tayari hata kidogo. Ninapata wasiwasi kidogo kuhusu kuwa Durban. Itachukua muda kabla ya kuwa Durban, " alisema.

"Ninapitia mengi zaidi. Sahau kuniona Durban. Sio kwamba hata mimi nina hasira na huko Durban. Ni ngumu tu. Ni miezi mitatu tu tangu Kiernan afariki, labda baada ya muda. Lakini nina matumaini kamwe nisibadilishe mawazo yangu."

"Nitamwambia nini Kairo siku ya Baba?"

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii