Chelsea Wamwajiri Mauricio Pochettino Kuwa Kocha Wao Mpya

Klabu ya Chelsea imemteua Mauricio Pochettino kuwa meneja wao mpya huku mzawa huyo wa Argentina akikabidhiwa kibarua kigumu cha kufufua Blues iliyokumbwa na masaibu tele. 


Pochettino alitia saini kandarasi ya miaka miwili na chaguo la nyongeza ya mwaka mmoja huku akirejea kwenye Ligi ya Uingereza miaka minne baada ya kutimuliwa na Tottenham. 


Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 51, ambaye alitambulishwa rasmi Jumatatu, Mei 29, alikuwa nje ya uwanja tangu alipofukuzwa na Paris Saint-Germain mnamo Julai 2022. "Mauricio ni kocha wa kiwango cha kimataifa mwenye rekodi bora. Sote tunatazamia kuwa naye kwenye bodi," wamiliki wenza wa Chelsea Todd Boehly na Behdad Eghbali walisema katika taarifa. 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii