Mbappe atasalia PSG mpaka mwakani

Kylian Mbappe amewahakikishia mashabiki kuwa atasalia kwenye Klabu hiyo atakipiga hapo mpaka mwakani na kuhitimisha tetesi zinazomuhusu kuondoka.

Mbappe, 24, ambaye ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligue 1 amewahakikishia kuwa bado yupo yupo sana tu.

Tuzo hiyo ni ya nne mfululizo kwa staa huyo ndani ya Ligue 1.

“Ni fahari jina langu kuacha alama kwenye historia ya ubingwa wa nchi yangu. Mwakani nitacheza Paris Saint-Germain bado nina mkataba.”- Mbappe

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii