NE-YO:SIPENDI KWENDA KUANGALIA MCHEZO WA NGUMI KWA WANAWAKE

Shaffer smith maarufu kwa jina la neyo ambaye ni msanii wa muziki wa rnb kutoka nchini marekani aliyefanikiwa kwa nafasi yake katika mziki kushinda na kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali kubwa ikiwemo grammy.

Neyo ambaye hivi karibuni aliingia katika vichwa vya Habari akidai kuwa anafurahia Maisha ya kuwa peke yake baada ya kutalakiana na mke wake.

Kwa mara nyingine akiwa katika mahojiano na mike Tyson neyo aliulizwa swali kama huwa anafurahia kuangalia mchezo wa ngumi kwa kufika katika tukio na kusema kuwa :-


“binafsi huwa sifurahii kuangalia ngumi za wanawake kwasababu nikishafika katika eneo la tukio huwa mara nyingi natazamia Zaidi walivyovaa na maumbile yao na sitazami namna ambavyo wanatumia mbinu katika upiganaji wao”

Alisema neyo ambaye pia ni moja kati ya msanii ambaye anakiri kuwa anafurahia Zaidi kuangalia ngumi hizo akiwa nyumbani kwake.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii