RICK ROSS AWEKA WAZI ANATARAJIA WATU ELFU SABA KATIKA SHOW YAKE YA MAGARI

Msanii wa muziki wa hiphop kutoka nchini marekani rick ross ambaye pia ni boss wa maybach music group.

Rick ross mwaka jana alifanikiwa kufanya show yake ya kwanza ya magari katika eneo la nyumbani kwake show ambayo ilihusisha magari mengi sana anayomiliki pamoja na magari ya watu wengine mbali mbali.

Mwaka huu msanii rick ross amepata kufanya tena show hiyo ya magari huku akiahisi kuwa itakuwa kubwa zaidi ya mwanzo kutokana na namna ambavyo wamejiaandaa kwaajili ya jambo hilo.Akizungumza na chanzo cha habari cha revolt rick ross amesema kuwa”mwaka huu natarajia kuwa na show kubwa sina uhakika na idadi ya watu itakuwaje lakini inaweza kufika elfu saba lakini kubwa la muhimu hii ni show ya watu wanaojitambua na nia ya kukua zaidi kifedha na kibishara” amesema rick ross.


Show hiyo itakuwa na muziki,chakula ,burudani pamoja na wageni na watu maarufu mbali mbali itafanyika june 3 kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 12 jioni katika makazi yake maarufu promise land huko georgia fayetteville nchini marekani.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii