Msanii na mwigizaji nick cannon kutoka nchini marekani ambaye mara kadhaa amekuwa akiingia katika vichwa vya Habari kutokana na namna ambavyo amekuwa akipata Watoto na wanawake tofauti tofauti kwa kufatana kitu ambacho kimekuwa mjadala kwa watu wengi kuhusu idadi ya Watoto ambayo ni kubwa .
Nick cannon aliwahi kufunga ndoa na mwanamuziki maraiah carey miaka kadhaa iliyopita ambaye waliachana kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wao,sasa wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu msanii huyo kwanini asiwe na mke .
Lakini katika mahojiano na revolt nick cannon ameweka bayana kuhusu mpango wa kuwa kwenye ndoa na kusema kuwa”mimi sipendi ndoa ndoa nzuri ni ya watu wawili ambao wanaweza kuanza Pamoja katika msingi na sio kwenda katika mtandao wa only fans”
Alisema nick cannon ambaye anaamini kuwa kwa nafasi yake yeye ni moja kati ya mtu ambaye anapenda lakini haipendi ndoa.