Bukayo Saka Atia Saini Mkataba Mpya na Arsenal

Mshambuliaji mahiri, Buyako Saka ametia saini mkataba mpya wa kusalia Arsenal hadi mwaka wa 2027. 

Akizungumzia mkataba huo mpya Saka alisema klabu hiyo ndiyo sehemu sahihi ya kupiga hatua inayofuata. Mshambuliaji huyo wa Uingereza amefunga mabao 14 kwa The Gunners msimu huu, na kutoa pasi 11 za mabao. 


Kinda huyo mwenye umri wa miaka 21, tayari ameichezea klabu hiyo mechi 178 na ameshiriki katika mechi zote za Ligi Kuu ya Arsenal katika kipindi cha kampeni mbili zilizopita. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii