• Jumatano , Agosti 13 , 2025

MAMA WA MSANII COSTA TITCH AVUNJA UKIMYA ADAI MAJIBU YA VIPIMO VYA SUMU

Mama mzazi wa msanii wa muziki kutoka nchini Africa ya kusini costa tich ambaye pia alikuwa anawakilisha titch gang aliyefariki mwanzo mwa mwaka huu march 12 huko afrika ya kusini akiwa anatumbuiza katika tamasha maarufu la Ultra festival.

Baada ya kuanguka na kupata huduma ya kwanza ambayo haikufanikiwa kuzaa matunda na taarifa kutangazwa kuwa msanii huyo alipoteza Maisha yake,ni jambo ambalo halikuwa rahisi kwa mashabiki na watu mbali mbali kufuatia kifo hicho ambacho kiliibua maswali mengi.


Mapema leo kupitia ukurasa wa isnatgrama wa marehemu costa tich mama yake mzazi aliandika ujumbe ambao umefanya watu wengi kushtuka kulingana na ujumbe unavyosema.

"Huduma za Kitaifa za Maabara ya Afya zinaweza kuchukua miezi au hata miaka kukamilisha vipimo vya sumu. Hii inamaanisha kuwa mimi sio mama pekee nchini Afrika Kusini ninayepaswa kusubiri majibu. Inamaanisha pia kama mtu yeyote alimpa mtoto wangu sumu, anaweza kuondokana na mauaji. Ninaomba msaada wa kupata majibu kwani hata polisi hawawezi kufanya lolote bila matokeo haya ya matibabu," Ameandika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii