Karen mukupa ni msanii wa muziki wa hiphop ,rap na raggae kutoka nchini Denmark ambaye alizaliwa nchini Zambia na kukulia nchini Tanzania mpaka alipofika umri wa miaka 15 na kuhamia nchini Denmark ambapo anaishi mpaka sasa.
Karen mukupa ni moja ya mwimbaji ambaye anaipenda kazi yake ya Sanaa kuanzia uandishi wa kazi zake Pamoja na uwasilishaji wa kazi zake ambao hubeba maudhui ya aina mbali mbali yenye kufundisha pasi na kuburudisha jamii.
May 19 karen mukupa ameachia rasmi albumu yake ambayo ameipa jina la BONOBO album ambayo ina nyimbo 12 ndani yake ikiwemo,Indad,Monster,Omveje,Hvis du,Elsk,Hvid pige long deluxe version,Fi den er Erfaren,Fucciboi,Ondt af mig sel,ÆGTE ft Skyggesiden,Omveje radio edit and Hvid pige radio edit.
Album ya BONOBO ambayo imezungumzia mambo mbali mbali inapatikana katika vyanzo mbali mbali vya kusikiliza muziki kama vile spotify,itunes na nyingine nyingi.
https://music.apple.com/dk/artist/karen-mukupa/305731070