Davido 'Kumpata Chioma na Kuwa Naye ni Auamuzi Sahihi

Msanii  David Adeleke (Davido) ameeleza kuwa moja kati ya uamuzi bora zaidi kuwahi kuufanya ni kumpata mke wake Chioma.

Kupitia mahojiano na kituo cha Redio, Beat 105.3 FM cha mjini Atlanta, Marekani Davido amesema alifahamiana na mke wake takriban miaka 20 hali iliyopelekea maelewano mazuri baina yao.

“Mimi na mke wangu (Chioma) tulikua pamoja na tulikwenda shule pamoja, nilikutana naye chuoni nikiwa mwaka wa kwanza na tumezoeana sana tu, Yeye ni kama sehemu yangu."

“Hakika lazima upate mtu anayekuelewa, kwangu uamuzi bora zaidi ambao nimewahi kufanya ni kuwa nae kwani nimemfahamu karibu miaka 20."

Wawili hao walifunga ndoa miezi kadhaa iliyopita baada ya kifo cha mtoto wao wa kiume, Ifeanyi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii