Huenda Simba SC ikawakosa Aishi Manula na Sadio Kanoute katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo Keshokutwa Jumamosi (April 22) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kuanzia saa kumi jioni.
Malinda Lango Manula na Kiungo Kanoute wakikosekana katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans uliopijwa mwishoni mwa juma lililopita (Jumapili-April 16), ambapo Simba SC ilishinda 2-0.