ROONEY ATAJWA KUINOA EVERTON

Nyota na mkongwe wa Manchester United, Wayne Rooney anatajwa kuwa huenda akarithi mikoba ya Rafael Benitez
ndani ya Goodison Park.
Everton siku ya Jumapili ilimfuta kazi aliyekuwa kocha wake Rafael Benetiz baada ya timu hiyo kuendelea kufanya vibaya ndani ya Premier League.
Ushindi wa Norwich City wa mabao 2-1 dhidi ya Everton ndiyo ulipelekea kibarua cha kocha huyo kuota nyasi,baada ya kocha huyo kudumu hapo kwa miezi sita tu.
Inaelezwa kuwa kocha huyo hakupewa fedha za kutosha kwaajili ya kufanya usajili kwani katika mechi 12 zao za mwisho alipoteza tisa. Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuondolewa Benitez, Rooney ndiye ambaye kwa sasa anainoa Derby County ya Championship ndiye anatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kutua kwenye kikosi hicho.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii