Watu waandamana Senegal dhidi ya kesi dhidi ya kiongozi wa upinzani inaendelea

Darzeni ya waandamanaji wamekamatwa na polisi katika mji mkuu wa Dakar nchini Senegal, wafuasi wa upinzani wakishutumu mashtaka dhidi ya kiongozi wa upinzani, wanayosema yana lengo la kumzuia kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Wandamanaji waliwarushia polisi mawe na kufunga barabara huku wakiwasha moto barabarani. Polisi wamewarushia vitoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.

Kundi moja la waandamanaji lilizingirwa na polisi na walijaribu kujificha katika nyumba za watu lakini polisi wlaiwafuata ndani ya majengo na kuwaondoa.

Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, anakabiliwa na mashtaka kwakumshutumu waziri wa utalii, kwa ubadhirifu wa fedha.

Pia anakabiliwa na mashtaka tofauti ya kumbaka mfanyakazi katika duka la urembo.

Mandamano makubwa yalitokea mwezi March mwaka 2021 na kupelekea vifo vya watu 14, Sonko alipokamatwa kwa madai ya ubakaji.

Wafuasi wake wanasema kwamba madai dhidi yake ni njama ya ili kumzui katika juhudi zake za kugombea urais.

Mafall Sall, amekuwa miongoni mwa waandamanaji. Ana umri wa miaka 20

"Tumekuja hapa kuikomboa demokrasia yetu. Tumechoka. Tumeamua kuandamana kwa sababu tunaona Macky Sall hataki mazungumzo au kuheshimu uchaguzi. Anachojua ni madaraka."

Maandamano yalianza March 14 na yamekuwa yakiongezeka.

Kulingana na shirika la Amnesty international, zaidi ya wandamanaji 130 wamekamatwa kati ya March 14 na 16. Waandamanaji 3 wamefariki.

Hawa Ba ni kiongozi wa kundi la kutetea demokrasia Afrika magharibi la Open society initiative.

"Tunaendelea kushuhudia ongezeko la watu kukamatwa wakishiriki maandamano au kuukosoa utawala wa rais Macky Sall kwenye mitandao ya kijamii. Lakini pia, kwa sababu wanatumia haki yao ya kujieleza kupitia maandamano. Hili halijawahi kutokea."

Rais Macky Sall hajatangaza iwapo atagombea muhula wa tatu wa uongozi katika uchaguzi wa mwaka ujao, hatua ambayo imewakasirisha raia wengi wa Senagl.

Sall, amefanya marekebisho kwenye katiba ya nchi kuhusu muhula wa rais kuhudumu na wengi wana wasiwasi kwamba huenda anajitayarisha kugombea muhula mwingine.

Viongozi wengine katika eneo hilo wametumia mbinu za kijeshi kubakia madarakani.

Adbdul Diop ni mwaandamanaji.

"Nimekuja hapa kupinga dhidi ya ukosefu wa haki uliotawala Senegal, kupambana na udikteta wa rais Macky Sall. Senegal inaingia katika utawala wa kidikteta. Hiyo ndio sababu nipo hapa. Tupo tayari kufa."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii