Mwana FA" Vipengele vya kipuuzi, vya kinyonyaji viondoke, sitaki kusikia"

Naibu Waziri wa Sanaa Hamis Mwijuma maarufu kama mwanaFA amelitaka Baraza la Sanaa la Taifa basata.

Tanzania kusimamia kikamilifu mikataba kati ya wasanii na kampuni za kuuza nyimbo mitandaoni kwa madai mikataba yao inakuwa na mapungufu.

MwanaFA ametolea mfano kwamba kuna moja ya mikataba kuna kipengele ambacho kinasema ukitokea mgogoro utaenda kusikilizwa nje ya nchi.

Amewataka BASATA kuwa wakali na yeye atatafuta msaada wa kisheria ambao utasaidia baadhi ya changamoto za wasanii kunyonywa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii