Wanafurahia habari zangu mbaya kuliko nzuri- Hassan Mwakinyo

Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo amesema kuwa kuna watu wanaamini wao wanajua zaidi kuliko waliyopo kwenye tasnia ya Ngumi yenyewe huku akidai wapo baadhi ya waandishi ambao wana furahia zaidi habari zake mbaya kuliko nzuri.

Mwakinyo ameyasema hayo Machi 27, 2023 wakati akitangaza pambano lake dhidi ya Kuvesa Katembo kutoka Afrika Kusini litakalopigwa Aprili 23, 2023 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

”Kuna watu ni katika waandishi ambao wana furahia zaidi habari zangu mbaya kuliko nzuri, yani kuna watu nikishinda pambano wanaweza wasiandike kama nikiwa nimefiwa ama nimepoteza pambano, kwa sababu ndiyo habari ambayo inauza kwao.”

Mwakinyo ameongeza ”Lakini kuna namna unatoa habari kiasi kwamba ukiisoma unahisi huyu mwandishi mbali tu kuwa ni mwana habari lakini ana kitu cha ziada na mimi kwenye moyo wake.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii