Valangati la kuuzwa Manchester United

Imeelezwa kuwa mmiliki mwenza wa kutoka Familia ya Glazer, Avram Glazer hataki klabu ya Manchester United ipigwe bei kwa mujibu wa ripoti, licha ya klabu hiyo kuwekwa sokoni.

Klabu ya Man United imewekwa sokoni kwa Dau la Pauni Bilioni 6 na tayari wawekezaji wawili, Sir Jim Ratcliffe na Sheikh Jassim wameweka ofa zao mezani.

Mbali na wawekezaji hao, kuna kampuni nyingine ya Elliot pia imevutiwa na kutaka kuwekeza katika klabu hiyo, kwa makubaliano ambayo yatawawezesha Familia ya Glazers kudhibiti kila kitu jambo ambalo Avram anaunga mkono uwekezaji.

Avram anataka waendelee kuidhibiti klabu hiyo hata kama wataiuza ndio maana Mmarekani huyo alikuwa anasuasua kukubaliana na wazo la kuipiga bei klabu hiyo.

Inasemekana Avram mwenye umri wa miaka 62, alikuwa akifanya uchunguzi kuona ni kiasi gani familia yake inaweza kupata faida endapo Man United itakakuwa imeuzwa, vilevile hata kaka yake Joel mwenye umri wa miaka 55 alisuasua katika kuku- baliana na mpango huo.

Siri imefichuka kwamba Avram litaka afahamu kama Man United ina thamani ya Pauni 6 bilioni iliyotajwa na familia yake kabla ya kupigwa bei ndio maana alikuwa anasita kukubaliana na maamuzi ya familia yake moja kwa moja.

Imethibitishwa Ratcliffe na Sheikh Jassim wameweka ofa mezani zenye thamani ya Pauni 5 bilioni kila mmoja huku kukiwa na mipango mingine ya ziada, kwaajili ya maendeleo ya klabu ikiwemo kuwekeza katika usajili wa wachezaji wapya.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii