Aliyekuwa Kiungo Nyota wa Arsenal Mesut Ozil Astaafu Soka Akiwa na Miaka 34

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal, Real Madrid na Ujerumani Mesut Ozil ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 34.


Akitoa tanggazo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ozil alisema kuwa imetimia wakati wa kuondoka kwenye fani ya soka baada ya miaka 17 huku majeraha yakichochea uamuzi wake.


"Imekuwa safari ya kushangaza iliyojaa nyakati na hisia zisizoweza kusahaulika. Nimekuwa na fursa ya kuwa mchezaji wa soka wa kulipwa kwa karibu miaka 17 sasa na ninashukuru sana kwa nafasi hiyo."Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii