Imefahamika kuwa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, wameanza mikakati ya kumnasa kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham ili kumsajili kwa msimu ujao wa 2023/24,
Man City inatajwa kuwa katika mawindo ya kumnasa Kiungo huyo kutoka England tangu mwezi Oktoba mwaka jana kwa mujibu wa ripoti.
Imeelezwa kiungo huyo alialikwa katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kupata suluhu dhidi ya Manchester City, timu hizo zilipomenyana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita 2021/22.
Kocha Pep Guardiola baada ya kumsaini Erling Haaland katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Man City inajiamini itafanikiwa kuipata saini ya Bellingham atakayeuzwa kwa kitita cha Pauni Milioni 130.