ACT kuandamana hadi Ikulu kwa Rais Samia

Mwenyekiti wa ngome ya vijana wa chana cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo, amesema kwamba anawakaribisha wananchi katika maandamano ya amani yatakayofanyika kesho Aprili 18, 2023, yatakayoanzia Manzese kuelekea Ikulu ya Dar es Salaam kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


 maandamano hayo ni ya amani na lengo la kuyafanya ni kumuunga mkono Rais Samia na kwamba achukue hatua dhidi ya wabadhirifu wa fedha za umma waliotajwa kwenye ripoti ya CAG.

"Kesho tarehe 18 tutafanya maandamano ya amani kuonesha hisia zetu dhidi ya wabadhirifu, kuonesha namna gani tunauunga mkono Rais kwamba achukue hatua dhidi yao na wawajibishwe sababu wanafuja fedha za wananchi," amesema Abdul Nondo

Aidha Nondo ameongeza kuwa, "Naamini polisi hawatatuzuia bali watakuja kutulinda maandamano yetu yataanzia Manzese kuelekea Ikulu kwa Rais Samia kupeleka ujumbe wetu tunaomba wananchi wajitokeze, maandamano haya ni ya kila mtu,".


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii