Msanii maarufu nchini Guinea Grand P amemtoka kidosho mwenye umbo kali Eudoxie.
Grand P na Eudoxie walikuwa wamezua gumzo mitandaoni na penzi lao moto huku picha za mahaba yao zikipepea mitandaoni.
Licha ya tofauti kubwa za kimaumbile baina yao, penzi lao liliendelea kushika kiwango cha Grand P hata kuchora Eudoxie mkononi. Mjadala ulikuwa kuhusu umbo la Eudoxie ambaye ni mnene akilinganishwa na Grand P ambaye ni mfupi kama nyundo.
Hata hivyo, Grand P alipuuza tetesi zozote akisema 'Gari ni gari kwa dereva' na kiti ni pale pale kwa mwendeshaji yeyote. ,Msanii huyo alibarikiwa na maneno matamu ambayo alitumia kumpapasa Eudoxie huku akimpa penzi kwa straa. "Mpenzi wangu Eudoxie, wewe ndiye mrembo zaidi euniani. Nitaliandika jina lako kwenye moyo wangu ili nikufikirie maishani mwangu. Furaha yangu ni kuwa nawe. Wewe ndiye mpenzi wa maisha yangu," alimwambia Eudoxie wakati mmoja.