Sierra Leone yapiga marufuku mikutano ya siasa ya barabarani

Serikali ya Sieraa Leone Jumatatu imetangaza kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya mitaani ambayo kwa muda mrefu imetumika kwenye kampeni za uchaguzi, ikiwa imebaki chini ya miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa Rais.

Kwa mijibu wa shirika la habari la AFP, Tume ya kitaifa inayoratibu vyama vya siasa kupitia taarifa imesema kwamba ”nyakati za uchaguzi siyo ya kucheza dansi na kusherehekea, bali ni wakati wa kutafakari kuhusu masuala muhimu.”

Kwa kawaida, vyama viwili vikuu nchini humo- Sierra Leone People’s Party SLPP kinachotawala, pamoja na All People’s Congress APC, huwa vikifanya mikutano ya hadhara ambayo hupitia kwenye barabara za miji.

Kwa mujibu wa sheria mpya iliyotangazwa, vyama vya kisiasa sasa vitalazimika kutafuta mahala pa kufanyia mikutano yake kama vile viwanja vya michezo au vituo vya umma, ili kufanya mikutano ya kisiasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii