Kocha wa Chelsea Atimuliwa

Klabu ya Chelsea imemtimua Kocha wake Graham Potter baada ya muendelezo wa matokeo mabovu ya klabu hiyo huku jana Jumamosi akipokea kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Aston Villa.


"Chelsea ingependa kumshukuru Graham kwa juhudi zake zote na mchango wake na kumtakia heri kwa siku zijazo", taarifa ya klabu


Potter amejiunga na Chelsea akichukua nafasi ya Thoma Tuchel akitokea Brighton lakini hajaonesha ubora wowote ndani ya Chelsea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii