Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire akizungumza na Wadau wa usafiri kutoka Taasisi za Kikanda za Usafirishaji Majini (ISCOS), Jijini Dar es.
Nchi za Afrika zimetakiwa kuwekeza katika umilikiwa wa meli kubwa za kusafirisha mizigo kutoka nchi za Ulaya kuja Afrika kutoakana na ukauaji wa Biashara za Usafiri wa Majini duniani.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire kwenye mkutano uliowakutanisha wadau wa usafiri toka Taasisi ya kikanda inayohusu usafirishaji Majini (ISCOS).
“Usafiri kwa njia ya Maji ni mkubwa zaidi ya shehena ya Mizigo asilimia kumi duniani inasafirishwa kwa njia ya maji hivyo ni muhimu nchi za Afrika kumiliki meli ili tuweze kusafirisha mizigo”, alisema Migire.
Aidha, Migire ameongeza kwa kusema kuwa serikali na watu binafsi wakimiliki meli itasaidia sana wanafunzi wanaosomea ubaharia katika vyuo vyetu watakuwa na nafasi kubwa ya kupata mafunzo na uzoefu katika meli hizo hivyo ni muhimu nchi zetu kuwa na meli kubwa.
Mwakilishi kutoka kampuni inayotengeneza Meli hapa nchini Songoro Marine Godwin Isdori amesema kuwa Biashara ya Usafiri kwa njia ya Maji ni kubwa hivyo ni Muhimu kwa Afrika kumiliki Meli kwani Biashara hiyo inatoa ajira kubwa kwa vijana.
Kwa upande wake, Katibu mtendaji wa wamiliki wa Meli Afrika Bi. Funmi Folorunso kutoka Nigeria amesema ni muhimu kwa Serikali na watu binafsi kumiliki meli kwani ni usafiri unaotegemewa sana na kutoa wito kwa watu binafsi na Serikali za Afrika kuhakikisha zinamiliki meli ili waweze kusafirisha mizigo na kuweza kupata pesa za kigeni katika nchi za Afrika.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya kikanda inayohusu usafirishaji Majini (ISCOS) Daniel Kiyange amesema kuwa ni muhimu kwa waafrika kuwa na meli kwani taasisi hiyo kwasasa inaangalia namna mzuri ya kushirikisha nchi wanachama kununua na kumiliki meli
Taasisi ya kikanda inayohusu Usafiri Majini( ISCOS) inajumuisha nchi za Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda na Zambia.