Messi awanunulia zawadi ya iPhone wachezaji wa Argentina

Lionel Messi ametumia pauni 175,000 kuwanunulia zawadi za simu 35 aina ya iPhone rangi ya dhahabu wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina kutokana na mafanikio waliyopata ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia.

Nahodha huyo wa Argentina alitaka kuwapa wenzake zawadi hiyo kama sehemu ya kumbukumbu ya mafanikio waliyopata nchini Qatar na hivyo kuwachukulia simu kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Mkurugenzi Mtendaji wa iDesign Gold, Ben Lyons ameeleza namna Messi alivyomtaka kubuni zawadi hiyo maalum baada ya mafanikio waliyofikia huko Mashariki ya Kati.

Simu zote zimebuniwa sawa zikiambatanishwa na beji ya timu ya taifa Argentina ikiwekwa na nyota tatu juu zikiandikwa na jina la mchezaji husika na namba yake ya jezi sanjari na maneno ya ‘World Cup champions 2022’.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii