Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza rasmi kuwa Asiwaju Bola Ahmed Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC), ndiye mshindi wa Uchaguzi wa Urais wa Nigeria wa 2023.
Mwenyekiti wa INEC, Profesa Mahmud Yakubu, alitangaza kuwa Tinubu, ambaye ni gavana wa zamani wa Lagos, nduye mshindi wa uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali mapema Jumatano, Machi 1, jijiniAbuja. Alitangaza kuwa Tinubu alizoa kura 8,794,726 na kuwashinda wapinzani wake wa karibu, Atiku Abubakar wa Peoples Democratic Party (PDP) aliyepata kura 6,984,520 huku Peter Obi wa Labour Party (LP) akipata kura 6,101,533.
Awali, Tinubu alikimbia kortini kuzuia hatua za vyama vya upinzani kutaka matokeo ya uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali na kurudiwa, kwa madai ya kuwepo kasoro nyingi.Rais mteule na chama chake walikuwa wamewasilisha kesi ya kuzuia vyama vya Labour Party (LP) na Peoples Democratic Party (PDP) kusitisha kutangazwa kwa matokeo ya kura.