BAADHI YA NCHI AMBAZO TAYARI ZIMEINGIA 2022

Wakati Tanzania na baadhi ya nchi kote ulimwenguni ikiwa inahesabu saa kadhaa hadi kufika Januari 1, 2022, kuna nchi na miji tayari wamewasha fataki za 2022. Vilevile kuna miji ambayo huenda ikawasha fataki hizo wakati sehemu za ulimwengu kama Tanzania wakihesabu siku nyingine katika kalenda ya 2022.


Kwa ufupi hii ndiyo miji ambayo imeshafika 2022 na mingine inayokaribia kufika 2022. Kiribati, Kiritimati (Ijumaa Saa 7 mchana), Chatham Islands New Zealand (Ijumaa saa 7:15 mchana), Fiji- Urusi (Ijumaa Saa 9 Mchana), Queensland/ Australia (Saa 11:30 jioni), Japan, South Korea (saa 12 jioni).


Beijing, Hong Kong/China, Ufilipino, Manila, Singapore (Ijumaa saa 1 usiku) Hata hivyo, Mwaka Mpya wa Uchina kwa Mujibu wa Kalenda yao ni Feburuari 1, 2022.


Moscow/Urusi, Tanzania, Nairobi na nchi zingine 20 (Jumamosi saa 6 usiku). Cairo, Johannesburg/Afrika Kusini (Jumamosi saa saba usiku), Ujerumani na nchi zingine 45 (saa 8 usiku).

Nikujurishe tu pia kuwa Nchini Ethiopia, kwa mujibu wa kalenda yao, taifa hilo litakuwa linaingia 2014 kwa kuwa hadi sasa wapo 2013. Mwaka wa Ethiopia unaanza tarehe 11 Septemba au tarehe 12 Septemba katika mwaka wa Gregori.

Ethiopia wako nyuma miaka saba hadi minane ukilinganisha na miaka ya nchi kama Tanzania ambayo hufuata kalenda ya Gregori.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii