Uchaguzi Nigeria: Tinubu aongoza matokeo ya awali

Mgombea Urais wa Chama cha All Progressives Congress (APC), Asiwaju Bola Ahmed Tinubu kwa sasa anaongoza dhidi ya wagombea wa vyama vingine vya kisiasa katika Jimbo la Ogun, kutokana na matokeo ya uchaguzi wa maeneo ya Serikali za mitaa yaliyopokelewa hadi sasa.

Matokeo ya maeneo 10 ya serikali za mitaa yaliyotangazwa hadi sasa, Tinubu alifuatwa kwa karibu na mgombea wa Peoples Democratic Party (PDP), Atiku Abubakar.

Matokeo ya Serikali za mitaa yaliyotangazwa katika makao makuu ya Jimbo la Ogun ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC),  kufikia sasa ni: Remo Kaskazini, Ikenne, Egbado Kusini, Ewekoro na Abeokuta Kaskazini.

Mengine ni Ijebu Kaskazini, Ijebu Kaskazini-Mashariki, Imeko Afon, Odeda na Ijebu-Ode maeneo ya serikali za mitaa ambapo Kamishna Mkazi wa Uchaguzi (REC) wa jimbo hilo, Niyi Ijalaye alitangaza kuwa amefungua kituo cha kukusanya kura cha Jimbo la Ogun.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii