Floda grae ni moja ya mwimbaji wa muziki wa afro beat kutoka nchini afrika ya kusini ambaye amejikita zaidi nchini nigeria ambapo amekuwa akifanya shughuli zake za kimuziki akishirikiana na wasanii mbali mbali.
Hivi karibuni aliachia kazi yake iitwayo iyona le ambayo pia video ya wimbo huo inapatikana katika vyanzo mbali mbali vya muziki.
Floda grae yuko pia mbioni kuachia kazi nyingine mwaka huu kwani moja ya mpango wake ni kuachia kazi nyingi zaidi na kuendelea kukuza sanaa yake kwa ujumla.
Unaweza kumfatilia kupitia mitandao yake ya kijamii yaani instagram ,facebook,twitter @flodagrae ili kuwa karibu zaidi na kazi zake.