GABRIEL UNION:NILITAMANI KUSHEREHEKEA MIAKA HAMSINI NIKIWA AFRIKA.

Mwigizaji na mwanamitindo kutoka nchini marekani Gabriel union ambaye pia ni mke wa mcheza mpira wa kikapu mstaafu Dwayne wade ameweka wazi katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na jeniffer Hudson na kueleza kuhusu Safari yake ya afrika ilivyokuwa.

Gabriel alisema kuwa ilikuwa safari ambayo aliitamani sana na alitamani kushiriki na familia yake yote pamoja hivyo mwaka jana octoba 29 alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 50 na alisherehekea siku hiyo akifa barani afrika nchini Tanzania katika kisiwa cha Zanzibar huku akitarajia kuzulu mataifa mengine pia barani afrika ambayo aliyafikia ikiwemo Namibia na nchi nyingine ambazo alifanikiwa kuzifikia.


“Nilitaka kufurahisa siku yangu ya kuzaliwa ya miaka 50 nikiwa afrika na hata nitembelee nchi mbalimbali afrika kama ulivyo utaratibu wa familia yetu kufanya hivyo kila mwaka.

Alisema gabriel union ambaye amekiri kuwa safari hiyo ilikuwa safari nzuri sana ya kurudi kwenye asili yake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii